Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ivory Cost yaripoti kupona kwa mgonjwa wa Ebola tangu 1994

Ebola Case23 Ivory Cost yaripoti kupona kwa mgojwa wa Ebola tangu 1994

Sat, 28 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya nchini Ivory Coast, imetoa taarifa ya kwanza ya kupona kwa mgonjwa wa virusi vya Ebola aliyefikishwa katika moja ya hospitali nchini humo.

Taarifa Iliyotolewa nqa Msemai wa wizara hiyo, Serge Eholie, inaeleza kuwa kisa hicho ni cha kwanza kuripotiwa tangu mwaka 1994, hivyo kupona kwa mgonjwa huyo kunatoa matumaini mapya kwa taifa hilo katika kupambana na janga hilo.

"tumemfanyia vipimo mara mbili, na vyote vimeleta majibu yanayoonesha hana tena maambukizi, hivyo niseme kuwa hana tena maambukizi" Serge Eholie.

Hata hivyo, Shirika la Afya duniani, limewatambua watu wapatao 49 waliokuwa karibu na mgonjwa huyo katika kipindi alichogundulika kupata virusi hivyo, huku serikali nchini humo ikianzisha kampeni ya kuwataka wananchi kujilinda kwa kufuata masharti ya afya yaliyowekwa katika kupambana na mlipuko huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live