Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ivory Coast: Omba omba wapigwa marafuku mjini

Omba Omba Ivory Cost.png Ivory Coast: Omba omba wapigwa marafuku mjini

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan, imepiga marafuku omba omba kwenye mji huo katika kile inachosema ni hatua ya kujaribu kurejesha mpangilio wa mji.

Naibu gavana wa mji huo, Vincent N'cho Kouaoh, amesema aina yoyote ya omba omba imepigwa marafuku kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa raia pamoja na kurahisisha shughuli za trafiki na usafiri.

Mwaka wa 2013, wizara ya usalama wa ndani nchini humo, ilipiga marafuku omba omba katika makutano ya barabara lakini ilishindwa kutekeleza agizo hilo.

Mataifa mengine barani Afrika yamechukua hatua kama hii lakini utekelezwaji wake umeonekana kukawama.

Hatua hii imekuja baada ya mamlaka pia kwenye mji huo kubomoa vibanda ambavyo vilikuwa vimejengwa bila idhini.

Abidjan ni mojawapo wa miji yenye idadi kubwa ya raia barani Afrika, ikiwa na wakaazi milioni sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live