Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Iran kuomboleza kwa siku tatu baada ya mauaji ya Haniyeh

Hamas Teharan.jpeg Iran kuomboleza kwa siku tatu baada ya mauaji ya Haniyeh

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Iran imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia mauaji ya kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran, huku ibada ya wafu ikitarajiwa kufanyika Alhamisi.

Kundi hilo la Hamas, limesema Haniyeh atazikwa siku ya Ijumaa nchini Qatar baada ya kufanywa kwa sala ya mazishi siku ya Ijumaa.

Wakati huo huo, Iran imesema kwamba Marekani ni ya kulaumiwa katika mauaji ya Haniyeh kwasababu ya kuiunga mkono Israel.

Kwa upande wake, Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kujizuia kwa pande husika na kuonya kuwa hakuna taifa litakalonufaika kutokana na mzozo mkubwa zaidi wa kikanda.

Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh auwawa Iran

Hamas imesema kiongozi wake aliuawa katika shambulizi la Israel mjini Tehran wakati Haniyeh alipokuwa katika ziara mjini Tehran kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian.

Hata hivyo Israel bado haijazungumzia tukio hilo.

Iran na Hamas zimetangaza kulipiza kisasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live