Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ingabire Victoire aishitaki Rwanda EAC

Ingabire Victoire (12).jpeg Ingabire Victoire.

Wed, 1 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasiasa wa upinzani wa Rwanda Mwanamama Ingabire Victoire ameishitaki Rwanda katika Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya serikali kumnyang’anya haki yake kama raia wa nchi.

Hatua hii inakuja baada ya mwezi March mwaka huu, Mahakama Kuu mjini Kigali kumnyima haki yake kama raia na kupoteza nafasi ya kuombea urais wa Rwanda.

Mwezi wa Februari mwaka huu, Ingabire Victoire alikuwa amekata rufaa akiomba kurejeshewa haki yake baada ya kupita miaka mitano akiwa amepewa msamaha na Rais wa Rwanda.

Kiongozi huyo wa chama cha kisiasa cha upinzani DALFA amesema kuwa ana imani kama atapata haki yake katika Mahakama hiyo ya Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live