Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

India yataka Afrika ipatiwe uanachama G20

India Waziri Mkuu India yataka Afrika ipatiwe uanachama G20

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amependekeza kwamba, Muungano wa Afrika (AU) upate uanachama kamili katika Kundi la 20 (G20) wakati wa mkutano wa kundi hilo mjini New Delhi mwezi ujao.

Akizungumza Jumapili katika Mkutano wa Biashara wa 20 huko New Delhi, Modi amesema: "Tuna maono ya ushirikishwaji na kwa maono hayo, tumealika Muungano Afrika kuwa mwanachama wa kudumu wa G20,"

Kando ya mkutano wa kilele wa BRICS siku ya Alhamisi huko Afrika Kusini, Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil alisema BRICS inaunga mkono kujumuishwa Muungano wa Afrika katika Kundi la mataifa ya G20.

Wakati Mkutano wa G20 unakaribia Septemba 9-10, Modi amesema kuwa wakuu wa nchi 40 na mashirika mengi ya kimataifa watafika katika mji mkuu wa India kushiriki katika mkutano huo, ambao utakuwa "ushiriki mkubwa zaidi katika historia ya G20.”

G20 mwaka huu pia ilialika nchi tisa zisizo wanachama "wageni", zikiwemo Bangladesh, Singapore, Uhispania na Nigeria, kando na mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya Duniani, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.

G20 ni kongamano la kiserikali la nchi zilizoendelea na zinazoendelea ambazo zimepiga hatua kubwa kiuchumi duniani. Kundi hilo linajumuisha nchi 19 na Umoja wa Ulaya (EU).

G20 inajumuisha karibu asilimia 85 ya Pato la Taifa (GDP) duniani, zaidi ya asilimia 75 ya biashara ya kimataifa, na karibu theluthi mbili ya watu duniani - lakini Afrika Kusini ndiyo pekee mwanachama kutoka bara Afrika.

India kwa sasa inashikilia urais wa G20, nafasi ambayo inazunguka kila mwaka kati ya nchi wanachama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live