Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inasikitisha: Mama abakwa na wanaume 7 mbele ya mwanae "Natamani kufa"

Wnanaume Saba Rape Asimulia jinsi alivyobakwa na wanaume saba mbele ya mwanae

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika ukumbi wenye giza mjini Bumako nchini Mali watu wanasimulia mambo mazito na ya kutisha yaliowakumba amabyo mengi yaliyotokana na mzozo wa muda mrefu nchini humo wakati wakikabiliana na machafuko ya kisiasa .

Mchakato wa ukweli na upatanisho nchini humo unasaidia karibu waathiriwa 30,000 wa ghasia kutoa ushuhuda wao unashudiwa na simulizi hii ya kusikitisha ya mwanamama huyu.

Wiki iliyopita mwanamke aliyejifunika pazia alisimama kusimulia maswahibu ya kubakwa na wanaume saba mbele ya mwanae wa kumzaa.

"Siku waliochukua ubalozi mdogo wa Algeria, usiku wanaume saba walivamia nyumbani kwetu na kutufunga sebuleni, walipoamua kutubaka niliwasihi wamuepushe mwanangu kwenye eneo la tukio lakini walikataa, nilimuomba mtoto afumbe macho"

"Lakini pamoja na kuwasihi wabakaji kuhusu kumuepusha mwanangu hawakutaka kuniskiliza" Amesema mwanamke huyo ambaye jina limehifadhiwa.

Kwasasa mwanamke huyo anatamani kifo zaidi kuliko kuishi kwani kitendo alichofanyiwa kimeleta athari kubwa kwa familia yake hadi kupeleka kuathiri afya ya mwanae.

"Walimlazimisha mwanangu mdogo kutazama tukio la ubakaji, kwa jumla wanaume saba walinibaka mbele ya kijana wangu, watatu weupe na wanne weusi"

"Leo napendelea kifo kuliko kuishi, na baada ya hapo walichukua mali zetu kisha mwanangu alimfungua baba yake kamba na tangu siku hiyo mume wangu alitoweka na hajawahi kurejea tena nyumbani, sijui wapi alipo huu ukiwa ni mwaka wa 10"

"Mwanangu pia amepata matatizo ya akili kufuataia tukio hilo amekuwa akikimbia kila napo niona hadi saa" Amesema mwanamke huyo kwa uchungu.

Shambulio hilo lilitokea mwaka 2012 katika mji wa kaskazini wa Ghao ambao uliangukia mikononi mwa wapiganaji wa Jihad

Chanzo: www.tanzaniaweb.live