Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inasikitisha! Kijana aliyepondwa na kusagwa kwenye tanuru la moto kuzikwa leo

Marehemu Otieno Otieno kuzikwa leo

Sat, 9 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Caleb Otieno aliyepondwa na kuchemshwa hadi kufa katika tanuru la kuyeyushia vyuma kwenye kiwanda cha kampuni ya Blue Nile Rolling Mills mjini Thika atazikwa nyumbani kwao eneo la Kogony katika Kaunti ya Kisumu leo Jumamosi, Aprili 9,2022.

Mabaki ya mwili wake yalitolewa katika hifadhi moja ya maiti mjini Thika jana Ijumaa na kusafirishwa hadi nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.

Otieno alikuwa akifanya kazi ya ukibarua cha kuweka vipande vya chuma katika moto mkali katika kampuni hiyo ambapo siku ya kifo chake, Machi 25,2022 alikuwa kazini kama kawaida.

Inaarifiwa dakika chache kabla ya kifo chake, alimpa mwenzake KSh 50 sawa na shilingi 1,000 za Tanzania ili amnunulie chakula cha mchana. Mfanyakazi mwenzake aliporudi na chakula hicho, Otieno hakuwepo tena eneo hilo. 

Inaelezwa kuwa, Otieno alipokuwa akiweka vipande vya chuma kupitia kinu cha cha tanuru ilo lenye mpto mkali, gloves zake zilikwama kwenye vyuma.

Hapo ndipo vinu vilipomvuta kwenye mashine ambayo ilimponda vipande vipande kabla ya kumwangusha katika tanuru lenye uji wa moto na kumuunguza vibaya hivyo kupoteza maisha.

DCIO wa kaunti ndogo ya Thika Joseph Thuvi aliambia gazeti la the Star kuwa walifika eneo la tukio na kukusanya chembechembe ambazo zilionekana kuwa vipande vya mifupa kutoka kwa tanuri hiyo. 

Kwa mujibu wa chapisho hilo, Thuvi alisema kuwa suala hilo litashughulikiwa tu kama kisa cha ajali za kawaida kazini.

Inaarifiwa kampuni hiyo imeiambia familia ya marehemu kwamba itakuwa ikiwalipa Ksh 7,000 kila mwezi kwa miaka mitano kama fidia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live