Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Imam Mkuu akamatwa na fuvu la kichwa cha binadamu

Mauaji Fuvu.png Imam Mkuu akamatwa na fuvu la kichwa cha binadamu

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Washukiwa watano wa matambiko ya itikadi kali akiwemo Imam Mkuu wa dini ya Kiislamu wameripotiwa kutiwa nguvuni na dola katika mjii mkuu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chombo kimoja cha habari nchini humo, Imam huyo na wenzake walikamatwa wakiwa na fuvu la kichwa cha binadamu na viungo vingine vya mwili wa binadamu.

Kasisi huyo na wengine wanne waliripotiwa kukamatwa na wakazi wa eneo la Adamo, Ikorodu, Jimbo la Lagos kabla ya kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi la Nigeria (NPF).

Mkazi mmoja na shuhuda wa tukio hilo aliyethibitisha hilo kwa gazeti la SaharaReporters siku ya Ijumaa alisema kuwa mmoja wa maulama wa Kiislamu alinaswa na fuvu la kichwa cha binadamu na kukiri kuwa alikuwa akifanya kazi kwa mkuu wake, aliyetambulika kwa jina Imam Babalola.

Mkazi huyo aliongeza kuwa washukiwa hao walizuiliwa na Kitengo cha Polisi cha kupinga utekaji nyara na wafuasi wa dini katika Araro Adamo Jimbo la Lagos siku ya Alhamisi.

"Nimemfahamu Imam kwa zaidi ya miaka 5 na huyu ni mtu ambaye jamii nzima inasimama nyuma kusali, mtu ambaye wengi wetu tunamtazama," chanzo kilisema.

“Watu waliwakamata watu wake wakiwa na kichwa na baadhi ya sehemu za binadamu, alikiri kwamba alikuwa amezishikilia kwa ajili ya Imamu. Hapo ndipo watu walipovamia nyumba ya Imam na kumkamata pamoja na watu wake wanne,” kiliongeza chanzo.

Haya yanajiri miezi mitatu tu baada ya mhubiri wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 45 kukamatwa na Polisi wa Nigeria, Kamandi ya Jimbo la Oyo, kwa madai ya kupatikana na viungo vya mwili vilivyovunwa hivi majuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live