Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ilichosema Rwanda kesi ya Kabuga kusitishwa

Kabuga Rwanda Ilichosema Ilichosema Rwanda kesi ya Kabuga kusitishwa

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Rwanda kupitia msemaji wake, Yolande Makolo, imetangaza kwamba uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya mahakama ya kimataifa kusitisha kesi ya Kabuga Félicien, ni wa kusikitisha kwa waathiriwa wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi, lakini kwamba Rwanda inaheshimu uamuzi huo.

Wakati huo huo mwendeshamashtaka wa mahakama hiyo Serge Brammertz naye amesema kwamba uamuzi wa mahakama ya rufaa lazima uheshimiwe, hata ikiwa matokeo hayaridhishi.

Msemaji wa serikali ya Rwanda,Yolande Makolo ameviambia vyombo vya habari mjini Kigali kwamba Rwanda inaheshimu uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Rufaa wa kusimamisha kwa muda usiojulikana kesi ya mshukiwa mkuu wa mauaji ya kimbari Felicien Kabuga akisisitiza kwamba, sio jambo la kufurahisha kwa manusura wa mauaji hayo na kusema kwamba ‘’kwa vyovyote vile Kabuga bado ni mshukiwa wa uhalifu mkubwa."

Awali jumuiya ya manusura wa mauaji ya kimbari IBUKA ilitangaza kusikitishwa na uamuzi huo wa mahakama ya rufaa kuamuru Kabuga aachiliwe huru.

Jumuiya hiyo imelaani ilichokitaja kuwa ‘’aibu kwa sheria ‘’ya kimataifa na kutowatendea haki manusura wa mauaji ya kimbari na kuiomba serikali ya Rwanda kusitisha ushirikiano na mahakama hiyo.

Mwezi Juni, majaji katika mahakama ya uhalifu wa kivita ya Umoja wa Mataifa waliamua kuwa Bw Kabuga hafai kufikishwa mahakamani kutokana na ugonjwa wa akili lakini walipendekeza taratibu mbadala zifanyike. Kwa sasa majaji wa rufaa wamekataa pendekezo hilo.

Kwa upande mwingine ,mwendeshamashtaka wa mahakama hiyo ya kimataifa Bwana Serge Brammertz kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema matokeo hayo yanatokana kwanza kabisa na Kabuga kukwepa mkono wa sheria kwa miaka mingi.

Alisema Kabuga akiwa na ufahamu kamili wa hatua zake kabla na wakati wa Mauaji ya Kimbari ya 1994, alikataa kushitakiwa mbele ya mahakama ya kimataifa iliyo huru na isiyopendelea upande kujibu mashtaka dhidi yake.

Ameongeza kwamba baada ya kupitia kwa makini uamuzi wa chumba cha rufaa ,’’ni lazima uamuzi huo uheshimiwe, hata ikiwa matokeo hayaridhishi’’.

‘’Uamuzi huu unaweza kuwa wa kukatisha tamaa, lakini ninaweza kuwahakikishia waathiriwa kwamba sio mwisho wa mchakato wa haki’’. Brammertz alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live