Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ikulu Kenya yatoa taarifa kuhusu kikao cha Rais na NASA

D59bd776d78de5e5 Ikulu Kenya yatoa taarifa kuhusu kikao cha Rais na NASA

Wed, 18 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ikulu imetoa taarifa kuhusu kikao cha Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wa upinzani Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Moses Wetangula na Musalia Mudavadi Mombasa

Msemaji wa Ikulu Kanze Dena alisema Rais alikutana na viongozi kadhaa wa vyama mbali mbali ili kujadili namna ya kukabiliana na maambukizi ya Covid-19.

Taarifa ya Kanze ilisema Rais ana hofu kuhusu kuongezeka kwa maambukizi pamoja na vifo vinavyoshuhudiwa.

"Viongozi hao wamekubali kuchukua nafasi na kuwashawishi Wakenya kuzingatia sheria za kukabili maambukizi ya Covid-19 pamoja na kukubali kuchanjwa," alisema Kanze



Ikulu ilisema viongozi hao walipongeza serikali kutokana na juhudi zake za kukabiliana na maambukizi ya maradhi hayo.

Picha zilizopakiwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Ikulu zilionyesha Rais akiwa pamoja na Raila, Kalonzo, Musalia na Wetangula.

Pia mawaziri Fred Matiang'i na Mutahi Kagwe walihudhuria kikao hicho sawa na maafisa wengine wa serikali.

Taarifa ziliibuka Jumanne Agosti 17 kuwa Rais alikuwa amewaita viongozi hao Mombasa wiki moja tu baada ya kufanya kikao cha kisiasa humo.





Duru ziliarifu kuwa Rais alitaka kukutana na vigogo hao ili kuwashinikiza kuungana na kuwa mgombea mmoja wa urais 2022.

Ombi lake kwao ni wawe na muungano ambao utakuwa na nguvu za kutikisa wimbi la naibu wake na kumbwaga.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke