Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Igathe afichua siri za kisiasa zilizomhusisha Chris Kirubi

89dc6c0568c9fd73 Igathe afichua siri za kisiasa zilizomhusisha Chris Kirubi

Fri, 18 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Igathe alisema tiketi yake na Mike Sonko 2017 iliundwa na Kirubi ambaye alimtaja kama bingwa mwenye akiliAlisema pia yeye ndiye aliishauri serikali ya kitaifa kuchukua usimamizi wa kaunti ya NairobiJamaa na familia walikutana Karen kumpa mkono wa buriani mfanyibishara huyo wa jijiniBinadamu akifa mengi hufichuka na hivyo ndivyo ilikuwa wakati wa misa ya kumuaga mfanyibiashara sugu wa jiji Chris Kirubi.

Aliyekuwa naibu gavana wa Nairobi Polycarp Igathe ndiye alitoboa siri kuhusu mkono wa Kirubi katika matukio ya kisiasa ambayo yamekuwa yakishuhudiwa jijini.

"Ni Kirubi ambaye aliunda tiketi ya Igathe na Sonko, yeye ndio aliunda na kutaka nitekeleze hilo," alisema Igathe kuhusu mwafaka wake wa kuchukua serikali ya Nairobi 2017.

Alimsifia Kirubi kwa kuwa bingwa mwenye akili nyingi kiasi cha kuipa serikali ushauri wa kisiasa kama vile jinsi ya kuongoza kaunti ya Nairobi.



Alisema ni yeye alishauri kuhusu serikali ya kitaifa kuchukua usukani wa kaunti ya Nairobi kupitia shirika la huduma za jiji NMS.

"Ni wakati pia nifichue lilikuwa ni wazo la Chris kuwa Nairobi irudi chini ya serikali ya kitaifa," alisema Igathe.

Jamaa na familia walijumuika katika kanisa la Evangelist Karen kumuaga Kirubi ambaye alifariki dunia baada ya kipindi cha kukabiliana na maradhiya saratani.



Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga na wenzake wa vyama vya Wiper na ANC Kalonzo Musyoka na Musalia Mudavadi ni miongoni mwa viongozi ambao walihudhuria ibada hiyo ya kumuaga Kirubi.

Viongozi wengine ni mkewe Naibu Rais William Ruto Mama Rachel Ruto, waziri wa michezo Amina Mohammed, seneta wa Bungoma Moses Wetangu'ula na waziri wa Utalii Najib Balala.

Kirubi aliaga dunia Jumatatu,Juni 14 baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa saratani, marehemu anatarajiwa kuzikwa Jumamosi, Juni 18 nyumbani kwake mtaani Thika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari za TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke