Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idriss Deby atangazwa mshindi Urais Chad

Screenshot 2021 04 20 At 14.00.27 660x400.png Idriss Deby atangazwa mshindi Urais Chad

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Tume ya Uchaguzi nchini Chad imemtangaza Idriss Deby wa chama tawala cha ‘Patriotic Salvation Movement’ (PSM) kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Urais uliofanyika tarehe 11 mwezi huu.

Deby amefanikiwa kutetea kiti chake hicho kwa 80% ya kura zote zilizopigwa. Tayari Rais huyo ameshaliongoza taifa hilo kwa kipindi cha takribani miaka 30 na katika uchaguzi huo ilikuwa ni kipindi chake cha sita kugombea nafasi hiyo.

Wakazi wa mitaa mbalimbali ya Mji Mkuu wa Chad, N’Djamene wameanza kusheherekea ushindi wa rais huyo mteule.

“TUSIKAE KWA KUSUBIRIA MATAMKO, RIPOTI YA CAG IMEONESHA”— MBUNGE MATIKO

Chanzo: millardayo.com