Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idara ya Hali ya Anga Yaona Kuhusu Mvua Kubwa Kaunti ya Nairobi

08a34cf34bcfba6b Idara ya Hali ya Anga Yaona Kuhusu Mvua Kubwa Kaunti ya Nairobi

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Idara ya hali ya anga nchini imeonya wakazi wa Nairobi dhidi mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha kuanzia leo Machi 30 hadi Aprili 5,2021.

Sehemu zingine za nchi zitakazo pata mvua nyingi ni pamoja na eneo la Ziwa Victoria, maeneo yote ya Bonde la Ufa, eneo la kati, Magharibi mwa nchi na Mashariki.

"Mvua hii iinaashiria wanzo wa msimu wa mvua mwaka huu. Hata hivyo kuwa uwezekano wa msimu wa ukame kuanza mapema" iIisoma taarifa Idara ya hali ya anga.

Maeneo kadhaa ya Kaskazini Magharibi na Kaskazini Mashariki huenda yakapokea upepo mkali zaidi.

Mvua ya asubuhi inatarajiwa maeneo ya Ziwa Victoria, huku ngurumo za radi na mvua ya rasha rasha ikitarajiwa adhuhuri. Mvua ya hapa na pale inatarajiwa alasiri.

Sehemu za nyanda za juu zinatarajia mawingu na mvua ya rasha rasha. Mvua kubwa inatarajiwa wakati wa alasiri sehemu hizo.

Kusini mashariki mwa nyanda za chini mvua inatarajiwa nyakati za asubuhi, hali hiyo itabisha majira ya mchana huku rasha rasha za hapa na pale zikitarajiwa majira ya jioni.

Maeneo ya Pwani mwa nchi Mombasa na viunga vyake mvua ya rasha rasha inatarajiwa asubuhi, mchana na jioni.

Idara ya hali ya anga imewasihi waendeshaji magari kuwa waangalifu barabarani ili kuepukana na ajali kutokana ha hali mbaya ya anga.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke