Utafiti mpya wa mamlaka ya kitaifa ya kupambana na matumizi mabaya ya pombe na madawa ya kulevya nchini Kenya (Nacada) unaonyeshakuwa matumizi ya mihadarati nchini humo yameibua wasi wasi mkubwa kuhusu kuennea kwa matumizi ya bangi miongoni mwa vijana wadogo.
Idadi ya watu wanaotumia bangi nchini Kenya ilikaribia kuongezeka maradufu katika miaka 5 - ripoti ya Nacada
Takwimu mpya zinaonyesha mienendo ya kushangaza katika kuanza na kutumia dawa za kulevya.
Zinaonyesha kuwa umri wa chini wa kuanza kutumia vilevi mbali mbali ikiwa ni pamoja na tumbaku pombe na madawa ya kulevya ni mdogo sana, hadi watoto wenye umri wa miaka sita wameingizwa katika matumizi ya tumbaku.
Imeonekana pia kuwa matumizi ya madawa ya kulevyakama vile heroni, huanza kutumiwa miongoni mwa watoto wenye umri mdogokuanzia miaka minane,na kumi na minne., wakati matumizi ya kokeini huanza katika umri wa miaka ishirini.
Ripoti hiyo inaangazia kuongezak karibu mara dufu kwa matumizi ya bangi katika ipindi cha miaka mitano iliyopita na hivyo kuibua wasiwasi kuhusu kuenea taarifa potofu na Imani potofu zinazohusu madhara yake., hususan miongoni mwa vijana.
Takwimu zilizotolewa na Nacada zilizoainishwa katika ropoti ya kina, zinaelezeazaudi kuhusu uzito wa tatizo hilo.