Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi ya waliouawa katika shambulizi la wanajihadi Burkina Faso yafikia 86

Burk Burkina Faso

Thu, 16 Jun 2022 Chanzo: BBC

Idadi ya vifo kutokana na shambulio la mwisho wa wiki la wanajihadi kaskazini mwa Burkina Faso imeongezeka hadi 86, mamlaka imesema.

Idadi ya awali ya shambulizi katika kijiji cha Seytenga ilifikia 79. Kiongozi wa jeshi la nchi hiyo Paul-Henri Damiba siku ya Jumatano aliahidi kuchukua hatua dhidi ya washambuliaji alipotembelea eneo la mkasa.

Burkina Faso imekuwa ikikabiliana na uasi wa wanajihadi tangu mwaka mwaka 2015 ambao umegharimu maisha ya maelfu ya watu na kukimbia karibu watu milioni mbili. Uvamizi wa hivi punde ni kikwazo kikubwa kwa serikali ya kijeshi, ambayo ililazimisha kuingia madarakani ikishutumu serikali iliyochaguliwa kwa kushindwa kushughulikia ukosefu wa usalama.

Mgogoro huo ambao pia unaathiri maeneo mengi ya Mali na Niger unazifanya jamii za vijijini kuyahama makazi yao na kuchangia uhaba mkubwa wa chakula.

Chanzo: BBC