Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko nchini Kenya yafikia 228

Idadi Ya Waliofariki Kutokana Na Mafuriko Nchini Kenya Yafikia 228 Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko nchini Kenya yafikia 228

Sun, 5 May 2024 Chanzo: Bbc

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na athari nyingine za mvua kubwa inayonyesha nchini Kenya imeongezeka hadi 228, wizara ya mambo ya ndani ilisema Jumapili.

Mvua kubwa ambazo zimesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi kote nchini katika wiki za hivi karibuni zinatabiriwa kuwa mbaya zaidi mnamo Mei.

Katika taarifa yake, wizara hiyo ilisema mafuriko zaidi yanatarajiwa "katika maeneo ya tambarare, maeneo ya pembezoni na mijini wakati maporomoko ya udongo/matope yanaweza kutokea katika maeneo yenye miteremko mikali,na miinuko ".

Mafuriko hayo yameharibu nyumba, barabara, madaraja na miundombinu mingine katika eneo kubwa la uchumi wa Afrika Mashariki.

Takriban watu 164 wamejeruhiwa na hali mbaya ya hewa, wakati 212,630 wamelazimika kuyahama makazi yao, wizara hiyo ilisema.

Chanzo: Bbc