Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi ya waandamanaji waliouawa Sudan yafika 123

DB47F09A C1D4 4D3E A3EE 951B283D9339.jpeg Idadi ya waandamanaji waliouawa Sudan yafika 123

Sun, 22 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya waandamanaji walioauawa nchini Sudan na vikosi vya usalama katika maandamano ya dhidi ya wanajeshi wanaotawala nchini hyumo imefikia 123.

Ripoti zaidi zinasema kuwa, wengi waliouawa katika maandamano hayo ni wakazi wa mji mkuu Khartoum ambao umekuwa ukishuhudia maandamano makubwa zaidi ikilinganishwa na miji mingine ya nchi hiyo.

Jeshi la Sudan, likiongozwa na Burhan, lilinyakua madaraka Oktoba mwaka 2021, baada ya kumzuilia Waziri Mkuu Abdalla Hamdok na viongozi wengine wa kiraia na kuvunja serikali ya mpito ya mwaka mmoja pamoja na baraza tawala la kijeshi na kiraia lililoundwa baada ya kuondolewa madarakani Rais wa muda mrefu wa Omar al-Bashir.

Hatua hiyo iliibua hasira na hasira katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika na kuibua malalamiko ya kimataifa, likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Tangu wakati huo nchi hiyo imekumbwa na maandamano ambayo yamesababisha vifo vya watu 123 na mamia kujeruhiwa.

Wananchi wa Sudan wanaoandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum na katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wanaamini kuwa jeshi halitaondoka kikamilifu madarakani licha ya kufikiwa makubaliano hayo ya kisiasa, na ndio maana wanasisitiza kuendeleza maandamano nchini.

Waandamanaji hao wamekuwa wakitaka jeshi liachie madaraka na kujiondoa kwenye ulingo wa siasa kwa kukabidhi hatamu za uongozi kwa viongozi wa kiraia, uitishwe uchaguzi wa kidemokrasia na kutatuliwa matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi hyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live