Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi ya vifo yazidi kuongezeka Morocco

Idadi Vifo Vya Tetemeko Morocco Yaongezeka Hadi 1,037.jpeg Idadi ya vifo yazidi kuongezeka Morocco

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia tetemeko la ardhi nchini Morocco, idadi ya watu wanaokadiriwa kufariki dunia katika tetemeko hilo inakadiriwa kufika watu 2,900.

Wale walionusurika wamejiunga na timu ya uokozi ili kuendeleza juhudi za kuwatafuta manusura wengine. Vikosi vya uokoaji vimeendelea kufanya kazi ya uokozi bila kuchoka, hata usiku kucha.

Ni muhimu kukumbuka kwamba hili ni tukio baya zaidi kuwahi kuikumba nchi ya Morocco, Kaskazini mwa Afrika, tangu tetemeko la ardhi la mwaka 1960 lililoharibu mji wa Agadir na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live