Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi ya vifo Sudan vyakaribia 100 huku mapigano yakiendelea

Idadi Ya Vifo Sudan Vyakaribia 100 Huku Mapigano Yakiendelea Idadi ya vifo Sudan vyakaribia 100 huku mapigano yakiendelea

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Muungano wa madaktari wa Sudan umesema takribani raia 100 wamefariki katika mapigano kati ya jeshi na kikosi cha wanamgambo ambapo sasa ni siku yake ya tatu.

Wakazi waliripoti milio ya risasi katika mji mkuu, Khartoum siku ya Jumatatu, na mapigano pia yameshuhudiwa katika miji mingine ya Sudan.

Haijulikani ni wanajeshi wangapi wameuawa, lakini maiti zinaripotiwa kuachwa mitaani.

Mali na magari mengi yameharibiwa.

Viongozi wa kanda wanasema wanatarajia kusafiri hadi Sudan siku ya Jumatatu ili kujaribu kusitisha mapigano ambayo yamesimamisha shughuli zote za misaada.

Huku nchi ikiwa inakabiliwa na ukame mkali na inahitaji msaada mkubwa.

Chanzo: Bbc