Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi vifo vya mafuriko vyazidi kupaa

Mafukio Vifo 259 Idadi vifo vya mafuriko vyazidi kupaa

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko ambayo yameharibu eneo la pwani karibu na mji wa bandari wa Durban nchini Afrika Kusini imeongezeka hadi zaidi ya 250, maafisa wanasema.

Hapo awali ilikadiriwa kuwa takriban watu 59 walikuwa wamefariki katika jimbo la KwaZulu-Natal.

Nomagugu Simelane, waziri wa afya wa KwaZulu-Natal, aliambia shirika la utangazaji la eNCA la Afrika Kusini kuwa watu 253 wamefariki.

Shirika la habari la Reuters linasema maafisa wa mkoa sasa wameweka idadi hiyo kuwa 259.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live