Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibada ya wanajeshi wa Kenya waliofariki ajali ya helikopta kufanyika leo

Ibada Ya Wanajeshi Wa Kenya Waliofariki Ajali Ya Helikopta Kufanyika Leo Ibada ya wanajeshi wa Kenya waliofariki ajali ya helikopta kufanyika leo

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Jeshi la Kenya limethibitisha kwamba ibada ya wafu kuwakumbuka wanajeshi wote itafanyika Jumamosi Aprili 20 kwa heshima na muongozo wa kidini itakayoongozwa na viongozi wa kidini ambao pia ni wanajeshi.

Uchunguzi umeidhinishwa kubaini chanzo cha ajali ya ndege katika kaunti ya Elgeyo Marakwet iliyosababisha vifo vya maafisa 10 wa kijeshi akiwemo mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Francis Ogola.

Haya ni wakati maandalizi ya mazishi ya Jenerali Ogola yakiendelea, akiatarajiwa kuzikwa siku ya Jumapili huku maafisa wengine wawili waliofariki katika ajali hiyo wakizikwa siku ya Ijumaa

Rais William Ruto ameongoza ujumbe kutoka serikalini kuifariji familia ya jenerali Ogola.

Ibada fupi iliandaliwa nyumbani kwa Jenerali aliyefariki huku Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya Kenya akitoa taarifa yake kwa familia ambayo imetoa muelekeo wa marehemu kuhusu mazishi yake.

Chanzo: Bbc