Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IS yadai kukata vichwa watu 11 Nigeria

IS yadai kukata vichwa watu 11 Nigeria

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Abuja (AFP). Kundi la Islamic State limetoa video linayodai inaonyesha mauaji ya Wakristo 11 nchini Nigeria.

IS linasema kuwa mauaji hayo ni sehemu ya kampeni yao ya hivi karibuni ya kulipiza kisasi cha mauaji ya kiongozi wake na msemaji nchini Syria.

Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuwahusu waathirika, ambao wote walikua ni wanaume, lakini inasema walikuwa wamekamatwa katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Video hiyo ya dakika 56 ilitolewa 26 Desemba na Shirika la habari la IS Amaq.

Wachambuzi wanasema ni wazi video hiyo imetolewa kwa makusudi katika kuambatana na sherehe za Krismasi, kama ambavyo muuaji mmoja anasikika akisema “hizi ni salamu za Krismasi.”

Picha ilichukuliwa katika eneo la wazi lisilojulikana.

Mmoja wa mateka aliyekua katikati anaonekana akipigwa risasi na kufa huku wengine 10 wakisukumwa ardhini na kukatwa vichwa.

Viongozi wa IS, Abu Bakr al-Baghdadi na msemaji Abul-Hasan Al-Muhajir waliuawa nchini Syria mwishoni mwa Oktoba.

Hata hivyo, zipo taarifa kwamba Abu Bakr alijiua mwenye mwenyewe kukwepa kukamatwa na majeshi ya Marekani yaliyokuwa katika operesheni nchini Syria.

Jumapili, vikundi vya watu wenye msimamo mkali viliua watu sita na kuteka wengine watano wakiwa wawili wa mashirika ya msaada, baada ya kuteka magari kwenye barabara huu  katika eneo la Maiduguri katika Jimbo la Borno.

Shambulio kama hilo lilitokea Desemba 5, pale IS waliovalia kama wanajeshi wa Nigeria walisimamisha magari na kutapekua katika vituo vya ukaguzi karibu na Maiduguri.

Kundi hilo katika taarifa yake limesema wanajeshi sita na raia wanane, wakiwamo wafanyakazi wawili wa Msalaba mwekundu walikuwa miongoni mwa waliotekwa.

Wiki iliyopita kundi hilo lilionyesha video ya watu 11 wanaosadikika ni mateka.

Mmoja wa mateka hao wanayejitambulisha kama mwalimu anasema wote 11 walikuwa Wakristo na aliiomba Serikali ya Nigeria kuwezesha kuachiwa kwao.

Chanzo: mwananchi.co.tz