Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IS wakiri kuhusika shambulizi la Kampala

Is Ug Pic Data Kundi la IS lathibitisha kuhusika shambulizi Uganda

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Kiislam la IS limethibitisha kuhusika na shambulio la bomu katika mgahawa uliopo nchini Uganda lililotokea mwisho wa juma, shambulizi ambalo polisi nchini humo wameliita kuwa ni la kigaidi.

Wachunguzi wamesema kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 20 aliuawa katika shambulio hilo na wengine watatu wakiwa wamejeruhiwa vibaya katika tukio hilo lililotokea Kaskazini mwa Kampala.

Hata hivyo katika ujumbe waliotoa kupitia vyombo vyao vya habari, kundi hilo limesema kuwa linahusika moja kwa moja na shambulizi hilo na kuwa limeua watu wawili na kujeruhi wengine watano.

"Kikosi cha usalama kutoka kwa wanajeshi wetu kiliweza kufanya shambulizi hilo jirani kabisa na mkusanyiko wa maafisa wa jeshi la Uganda" ilisomeka taarifa hiyo ya IS.

Oktoba 8, Is ilithibitisha kufanya shambulizi la kwanza nchini Uganda kwa kulipua kituo cha polisi cha Kampala na kujeruhi wengi, taarifa ya tukio hili haikuwekwa bayana na vyombo vya usalama vya nchini humo.

Siku kadhaa zilizopita, Uingereza pamoja na Ufarana walitoa tahadhari ya uwepo wa matukio ya kigaidi nchini humo, na kuitaka Serikali kuwa makini hasa katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa.

Shambulizi kama hili lilitokea mwaka 2010 wakati wa Kombe la dunia na kuua watu wapatao 76 waliokuwa wamekusanyika kutazama mechi katika eneo la pamoja mjini Kampala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live