Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IOM yaweka mikakati kukabiliana na El Nino Somalia

Mvua Gys IOM yaweka mikakati kukabiliana na El Nino Somalia

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema kuwa, liko tayari kuisaidia Somalia kukabiliana na mafuriko adimu ya “Super El Nino” kabla ya kutokea nchini humo.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa la uhamiaji limesema katika taarifa yake iliyotolewa Mogadishu, mji mkuu wa Somalia kwamba: "IOM kwa sasa inatuma timu yake nchini Somalia na inajiandaa kutoa msaada wa dharura kote nchini humo kujiandaa kukabiliana na mafuriko ambayo imetabiriwa kuwa huenda yakaikumba nchi hiyo katika wiki chache zijazo."

Taarifa hiyo imetolewa baada ya Mkurugenzi Mkuu wa IOM, Amy Pope, kumaliza ziara yake nchini Somalia Jumanne wiki hii na baada ya kuchukua uongozi wa shirika hilo tarehe Mosi mwezi huu wa Oktoba. Somalia inakabiliwa na majanga mengi yakiwemo mafuriko na ukame

Amesema, ziara yake hiyo ya nchini Somalia ilikuwa na lengo la kuangalia jinsi IOM inavyoweza kuendelea kuisaidia serikali ya Somalia kukabiliana na changamoto zilizosababishwa na ukame wa hivi karibuni, mafuriko yanayoendelea na majanga mengine ya hali ya hewa.

Amesema: "Tunahitaji kukabiliana kikamilifu na uhamiaji wa lazima ambao umesababishwa na matatizo ya mazingira; kutoa msaada na ulinzi kwa wale waliohamishwa na hali mbaya ya hewa, kutafuta ufumbuzi wa kudumu na kurahisisha uhamiaji wa maeneo mengine wakati wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa sambamba na kuimarisha ustahimilivu na subira kwa jamii zilizoathirika."

Kwa mujibu wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa, zaidi ya Wasomali milioni 2.3 wamekimbia makazi yao ndani ya nchi hiyo humo kutokana na majanga yanayohusiana na hali ya hewa.

Taarifa ya shirika hilo pia imesema, Somalia ina zaidi ya wakimbizi wa ndani milioni 3.8 ambayo ni moja ya idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa ndani duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live