Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IMF na Benki ya Dunia zahitimisha mkutano wao nchini Morocco

World Bank (600 X 336) IMF na Benki ya Dunia zahitimisha mkutano wao nchini Morocco

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi wanachama wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) zimekubali kuongeza michango yao kwa wakopeshaji wa kimataifa na kuipa Afrika kiti cha tatu katika Bodi yake ya Utendaji.

IMF imezitolea wito nchi wanachama kuongeza ufadhili kwa taasisi hizo, ili ziweze kusaidia vyema serikali mbalimbali katika vita dhidi ya umaskini na mabadiliko ya tabia nchi.

Nadia Calvino afisa wa IMF ameeleza kuwa, tumekutana pamoja hapa Morocco kujadili umuhimu wa kukuza ukuaji jumuishi na endelevu kwa kuendeleza ajenda zetu za hali ya hewa na masuala ya dijitali. Ameongeza kuwa, hoja hizi zilikuwa miongoni mwa malengo yaliyotajwa ya mikutano ya kila mwaka ya IMF na Benki ya Dunia ambayo yamefikia hitimisho lake leo Jumapili.

Kristalina Georgieva Mkurugenzi Mtendaji wa IMF pia amesema katika mkutano huo kwamba: Wakati umefika wa kuwa kitu kimoja. Amesema, ni vigumu kufanikiwa katika hali ya mivutano na kwamba wamekamilisha mkutano wao wakiwa na malengo manne ambayo yote yameweza kuyatimiza. Mkurugenzi Mtendaji wa IMF

Ijapokuwa mgawanyo wa kura haujabadilishwa IMF imekubali kupanua Bodi yake kutoka wajumbe 24 hadi 25 ili kuipa nafasi ya ziada Afrika, ambayo hadi sasa inashikilia nafasi mbili. Mkutano wa IMF na Benki ya Dunia umefanyika kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika tangu 1973.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live