Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IMF: Uchumi wa Burundi utaimarika kwa 4.3% mwaka 2024

Uchumi Kupanda IMF: Uchumi wa Burundi utaimarika kwa 4.3% mwaka 2024

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetangaza kuwa uchumi wa Burundi unatarajiwa kukua kwa asilimia 4.3 mwaka wa 2024, ongezeko kubwa kutoka ukuaji wa 2.7% mwaka wa 2023.

Mtazamo huu ulioboreshwa unachangiwa na utendaji bora katika sekta ya kilimo, ambayo ina jukumu muhimu katika uchumi wa nchi, hasa kupitia mapato kutoka kwenye zao la chai na kahawa.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, IMF ilibainisha kuwa makadirio ya ukuaji huo yanaungwa mkono na uzalishaji thabiti wa kilimo, uwekezaji wenye tija na mageuzi yanayoendelea kufanyika.

Uhaba wa mafuta ulitatiza shughuli za kiuchumi nchini Burundi mnamo 2023, na nchi inapata ahueni baada ya miaka mingi ya mizozo na ukosefu wa utulivu wa kisiasa.

IMF imeonyesha kuwa mwishoni mwa mwaka jana, akiba ya fedha za kigeni ya Burundi ilifikia dola milioni 96.4. Rais Évariste Ndayishimiye wa Burundi

Afrika kwa ujumla ina moja ya viwango vya juu zaidi vya ukuaji wa uchumi duniani. Kulingana na Shiŕika la Fedha la Kimataifa (IMF), saba kati ya mataifa kumi yaliofanya vyema zaidi mwaka 2024 yanayotarajiwa ni ya Afŕika, sita kati yao kutoka sehemu ya Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live