Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ILO yapata bosi mpya wa kwanza Muafrika

Ilopic Data Waziri mkuu wa zamani wa Togo, Gilbert Houngbo

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri mkuu wa zamani wa Togo, Gilbert Houngbo amechaguliwa kuwa mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), na atakuwa Muafrika wa kwanza kuliongoza shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

Houngbo mwenye umri wa miaka 61 atamrithi mwanaharakati wa vyama vya wafanyakazi wa Uingereza Guy Ryder, ambaye ataachia ngazi mwishoni mwa Septemba mwaka huu baada ya kudumu kwa miaka 10 katika kazi hiyo.

“Ni heshima kubwa kwangu kuwa mwakilishi wa kwanza wa kanda ya Afrika kuchaguliwa kuongoza ILO baada ya miaka 103," Houngbo ameniambia baraza la Shirika mara baada ya uchaguzi kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live