Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGP Kenya atangaza kujiuzulu, Ruto aridhia

Koome X Ruto.jpeg IGP Kenya atangaza kujiuzulu, Ruto aridhia

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya, William Ruto, ameridhia barua ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo Japhet Koome kujiuzulu.

Inaelezwa kuwa hatua hiyo inakuja kufuatia mauaji ya vijana wanaojiita 'Gen Z' yaliyofanywa na polisi wakati wa maandamano ya kupinga muswada wa fedha pamoja na yale ya kupinga serikali iliyopo madarakani yaliyoenda kwa takribani majuma matatu.

Mara baada ya baadhi ya vijana waandamanaji nchini humo kuuawa kwa kufyatuliwa risasi na polisi huku wengine wakiachwa na majeraha ya risasi, wananchi pamoja na viongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja nchini Kenya walitoa rai kwa IG Koome kujiuzulu kwa kile walichokidai kuwa ameruhusu askari wake kufanya mauaji kwa vijana walioamua kuandamana kwa amani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live