Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGAD yaonya kuhusu itikadi kali na ukosefu wa utulivu wa kisiasa Pembe ya Afrika

IGAD Yaonya IGAD yaonya kuhusu itikadi kali na ukosefu wa utulivu wa kisiasa Pembe ya Afrika

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya IGAD imesema kuwa, kuongezeka makundi yenye itikadi kali na ukosefu wa utulivu wa kisiasa katika baadhi ya nchi za Pembe ya Afrika kunaweza kudhoofisha juhudi za kudumisha amani na usalama na pia kutatanisha vita dhidi ya uharamia na biashara ya madawa ya kulevya.

Mohammed Ali Guyo, mjumbe maalumu wa IGAD katika ukanda wa Bahari Nyekundu, Ghuba ya Aden na Somalia amesema kuwa, hali hiyo imechangiwa na ukame wa hivi karibuni uliosababisha maelfu kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao.

Amesema hayo baada ya kikosi kazi kilichoteuliwa na IGAD kubainisha changamoto na fursa zilizopo katika ukanda wa Ghuba ya Aden na Bahari Nyekundu na kuwasilisha ripoti yake kwa nchi nane wanachama wa jumuiya hiyo.

Afisa huyo mwandamizi wa IGAD pia ametoa mwito wa kuongezwa juhudi za pamoja kati ya nchi zote wanachama, kwani mabadiliko ya hali ya hewa yanatatiza maisha na kusababisha kuongezeka ukosefu wa usalama huku jamii zilizoathirika zikihangaika kutafuta chakula, maji na malisho. Somalia ilivyochakazwa na mapigano ya ndani

Naye Moi Lemoshira, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora ya Kenya amesema kuwa, ukosefu wa usalama katika eneo hilo umeathiri vibaya maendeleo, na kusababisha kuongezeka vitendo vya kigaidi na makundi yenye itikadi kali, hivyo kuna haja ya kuweko ushirikiano wa pamoja wa kupambana na mambo yote hayo.

Katika sehemu moja ya matamshi yake, Lemoshira amesema: Ghuba ya Aden na Bahari Nyekundu ni ukanda wenye uwezo mkubwa, lakini ukosefu wa usalama, mabadiliko ya kisiasa na kukosekana utulivu katika baadhi ya nchi wanachama wa IGAD kunakwamisha juhudi za kunufaika ipasavyo na uwezo huo.

Afisa huyo wa Kenya alipongeza jopo kazi la kuchunguza fursa na changamoto za eneo la IGAD akiongeza kuwa, ripoti yao itasaidia kutengeneza ramani ya njia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live