Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGAD yaipa Sudan Kusini mwezi kukaa sawa

0d56604bebdaccf2885d46e5ef5f8292 IGAD yaipa Sudan Kusini mwezi kukaa sawa

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VIONGOZI wa Muungano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Maendeleo Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika (IGAD) wameipa serikali ya Sudan Kusini mwezi mmoja kukamilisha kazi za mpito kabla hawajaingilia kati kusuluhisha.

Katika mkutano wa viongozi hao uliofanyika wiki iliyopita kwa mtandao, viongozi wa IGAD wametaka serikali ya Sudan Kusini kutoa fedha za lazima na misaada kutekeleza masuala ya ulinzi ya usalama wakati huu wa mpito.

Pia wametaka serikali kutoa misaada ya kifedha kwa Tume ya kuondoa na kupunguza silaha za kivita (DDRC) ili kutekeleza mchakato huo.

Taarifa ya IGAD imeeleza serikali inatakiwa kukamilisha masuala hayo kwa siku 30 hadi Agosti 13 mwaka huu na ikiwa hawajakamilisha Mwenyekiti wa IGAD ataingilia kati yaliyobaki.

Serikali imeomba misaada kutoka mashirika ya kimataifa kwa ajili ya utekelezaji wa masuala ya ulinzi na usalama lakini baadhi ya wafadhili wametaka serikali kutoa fedha hizo haraka.

Chanzo: habarileo.co.tz