Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGAD kusimamia mkutano wa kutatua mgogoro wa vita vya ndani Sudan

Sudan Jeshiiii Malalamikp IGAD kusimamia mkutano wa kutatua mgogoro wa vita vya ndani Sudan

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Uongozi la Sudan limetangaza kufikia makubaliano na Shirika la Kiserikali la Maendeleo ya Afrika Mashariki, IGAD, ya kuitisha mkutano wa dharura wa wakuu wa jumuiya hiyo kwa lengo la kuchunguza mgogoro wa ndani nchini Sudan.

Makubaliano hayo yametangazwa baada ya mazungumzo ya Jenerali Abdel Fattah al Burhan, mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan, na Ismail Omar Guelleh, Rais wa Djibouti ambaye ndiye Mwenyetiki wa sasa wa Jumuiya ya Kiserikali ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (IGAD), mjini Djibouti.

Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimejadili uhusiano wa nchi mbili na hali ya sasa katika vita kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Radiamali ya Haraka, RSF.

Baraza la Uongozi la Sudan limetangaza katika taarifa yake kwamba: Jenerali al Burhan amewasilisha ripoti kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu uliofanywa na RSF dhidi ya raia wa Sudan.

Akiashiria mazungumzo ya Jeddah chini ya upatanishi wa Saudi Arabia na Marekani ili kumaliza mzozo kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya RSF, mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan amesema: Tunaunga mkono suala la kusimamisha vita na kurejesha amani kwa ajili ya maisha ya watu wa Sudan.

Jenerali al Burhan pia amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa IGAD, Workneh Gebeyehu, na pande hizo mbili zimekubaliana kwamba mkutano wa wakuu wa shirika hilo utafanyika hivi karibuni katika mji mkuu wa Djibouti, ili kuwasiliisha ramani ya njia ya kumaliza mzozo wa ndani nchini Sudan.

Baada ya mazungumzo hayo, Katibu Mtendaji wa IGAD ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba: Nimezungumza na mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan kuhusu usitishaji wa kudumu wa mapigano kwa lengo la kuboresha hali ya kibinadamu na kuweka msingi wa kupata suluhisho la mwisho la kisiasa.

Maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi katika mapigano yanayoendelea kati ya majenerali wa jeshi la Sudan kwa ajili ya kuwania madaraka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live