Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IEBC yaidhinisha saini milioni 1.14 mpango wa BBI

562e7ed49db560e253e0b3ad8fe8d57a IEBC yaidhinisha saini milioni 1.14 mpango wa BBI

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeidhinisha saini milioni 1.14 kwa ajili ya Mpango wa Maridhiano (BBI). Saini hizo ni kati ya milioni 4.2 zilizokusanywa na timu ya BBI inayoongozwa na Chama cha Orange Democratic Movement mwaka jana, lakini ni watia saini 1,140,845 pekee waliopitishwa.

IEBC ilikuwa inahitaji kuidhinisha saini milioni moja pekee, hivyo inamaamisha kuwa muswada wa BBI utasambazwa katika mabunge ya kaunti 47.

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ilisema hatua hiyo inatokana na sura ya 257 (4) ya Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 kuwa watawasilisha nakala ya muswada wa BBI wa mwaka 2020 katika kaunti kwa miezi mitatu ili kupitiwa.

Endapo Bunge la Kaunti litapitisha muswada huo, Spika wa kaunti atawasilisha nakala yake kwa Spika kwa Bunge Kuu na cheti kuwa bunge lake limeridhia. IEBC ilihitaji Sh milioni 241 kwa ajili ya kufanya uhakiki wa saini kabla ya kufanya majadiliano na Hazina katika mahitaji yao mengine ya Sh milioni 97.3.

Chanzo: habarileo.co.tz