Mon, 30 Aug 2021
Chanzo: JamiiForum
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imesema zaidi ya watu 44,000 barani Afrika hawajulikani walipo na asilimia 45 kati yao ni Watoto.
Imeelezwa kuwa, takriban 82% ya watu hao wanatokea Mataifa 7 yanayokabiliwa na mapigano ya silaha. ICRC imesema Nigeria ina zaidi ya nusu ya idadi ya ambao hawajulikani walipo Afrika
Mataifa mengine yenye idadi kubwa ni Ethiopia, Sudan Kusini , Somalia, Libya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Cameroon.
Chanzo: JamiiForum