Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ICC yaamuru fidia ya $56m kwa wahanga wa kundi la waasi wa Uganda

ICC Yaamuru Fidia Ya $56m Kwa Wahanga Wa Kundi La Waasi Wa Uganda ICC yaamuru fidia ya $56m kwa wahanga wa kundi la waasi wa Uganda

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Waathiriwa wa mbabe wa kivita wa Uganda Dominic Ongwen wametunukiwa zaidi ya €52m ($56m; £44.5m) na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Amri hiyo inawahusu watu 50,000, wakiwemo askari watoto wa zamani na watoto waliozaliwa kutokana na ubakaji na ndoa za kulazimishwa.

Ongwen alikuwa kamanda wa waasi wakatili wa kundi la Lord's Resistance Army (LRA).

Kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 25 jela nchini Norway kwa makosa mengi ya kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Alitekwa nyara akiwa mtoto na kulazimishwa kujiunga na LRA lakini akaendelea kuwa mmoja wa viongozi wa kundi hilo maarufu la waasi.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake, hoja yake kwamba anafaa pia kuchukuliwa kama mwathirika ilikataliwa na mahakama.

Uhalifu huo ulifanywa na wapiganaji wake kaskazini mwa Uganda mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Chanzo: Bbc