Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huzuni baada ya choo kuporomoka na kuua mtu Kahawa West

Huzuni Baada Ya Choo Kuporomoka Na Kuua Mtu Kahawa West.png Huzuni baada ya choo kuporomoka na kuua mtu Kahawa West

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mwanamume mwenye umri wa miaka 28 alifariki baada ya choo kuporomoka alipokuwa akijikinga na mvua Kahawa Magharibi, Nairobi.

Kwa mujibu wa polisi, mtu wa pili aliokolewa kutoka kisa hichona kupelekwa hospitalini katika tukio la Jumanne jioni.

Wawili hao walikuwa wameenda kwenye choo hicho kilicho nje ya makazi yao mvua ilipoanza kunyesha na kuamua kujikinga humo.

Kulingana na mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei, choo hicho kiliporomoka huku wawili hao wakiwa ndani.

Peter Ndegwa, 45, aliokolewa akiwa hai huku Isaac Nyongesa akifariki na mwili wake kutolewa mwendo wa saa 7 usiku, kulingana na ripoti ya polisi.

Timu ya mashirika mbalimbali inayojumuisha polisi na timu ya kukabiliana na majanga kaunti ya Nairobi ilifanikiwa kuuchukua mwili wa marehemu uliokuwa umezikwa kwenye tope.

Bungei alisema choo hicho huenda kilibomoka kutokana na mvua kubwa inayonyesha jijini.

“Tunahimiza kila mtu kuwa makini na mvua. Tunakumbana na baadhi ya matukio ya kuzama kwa manyumba jambo ambalo linaweza kuepukika,” alisema.

Aliongeza kuwa wamepanga vikosi sehemu mbali mbali ili kutoa msaada kwa wanaoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Idara hiyo imeonya kuwa mvua itaendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini na kuomba mamlaka husika kuchukua hatua kukabiliana na athari hizo.

Chanzo: Radio Jambo