Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndo waziri mkuu mpya wa Burundi baada ya Bunyoni kutumbuliwa

Gervais Ndirakobuca Gervais Ndirakobuca

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la Burundi jana Jumatano lilidhinisha uteuzi wa waziri mkuu mpya baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuonya juu ya uwezekano wa mapunduzi dhidi yake Juma lililopita.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Usalama wa Umma na Maendeleo ya Jamii, Gervais Ndirakobuca amechukua nafasi ya Alain Guillaume Bunyoni kuwa waziri mkuu mpya, baada ya kuidhinishwa kwa kauli moja la Bunge la taifa hilo.

Kuondoka kwa Jenerali Alain Bunyoni katika kiti hicho kumejiri baada ya Rais Ndayishimiye, ambaye amekuwa mamlakani kwa zaidi ya miaka miwili sasa, kutoa tahadhari juma lililopita kuhusu uwezekano wa mapinduzi dhidi yake.

Kumekuwa na uvumi kuhusu kinyang’anyiro cha mamlaka kati ya Rais Ndayishimiye na waziri mkuu huyo.

Mageuzi haya ya uongozi wa mamlaka nchini Burundi yanatokea siku chache baada ya Rais Ndayishimiye kuwashutumu hadharani "wale wanaojiamini kuwa wana nguvu zote" na wana ndoto ya kufikia madaraka kupitia mapinduzi, kutoka wasaidizi wake.

Ndayishimiye alichukua hatamu za uongozi mwezi June mwaka 2020 baada ya mtangulizi wake Pierre Nkurunziza kufariki kiutokana na kile kilichotajwa na viongozi kuwa mshtuko wa Moyo.

Taifa hilo la Afrika ya Kati, lilikuwa limeghubikwa na migogoro mwaka 2015 baada ya Rais wa wakati huo Pierre Nkurunziza, kutangaza azma ya kuwania muhula wa tatu uongozini, licha ya wasi wasi kuibuliwa juu ya uhalali wa hatua hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live