Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndiye mfanyabiashara tajiri aliyeshinda Urais Zambia

3d3808225d410853dd79a2443c4f3a19 Hakainde Hichilema, maarufu HH, ni mfanyabiashara tajiri nchini Zambia

Wed, 18 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Hakainde Hichilema, maarufu HH, ni mfanyabiashara tajiri nchini Zambia aliyegeukia siasa hadi kuongozi kilichokuwa Chama kikuu cha upinzani nchini Zambia cha United Party for National Development (UPND).

Hichilema ambaye kulinganisha na watangulizi wake bado ni kijana, akiwa amezaliwa Juni 4, 1962, anakuwa Rais wa saba wa Zambia tangu nchi hiyo ipate uhuru wake mwaka 1964.

Alikuwa anawaambia wapiga kura kwamba wanahitaji mfanyabiashara aliyefanikiwa kuelewa jinsi ya kupata uchumi katika taifa lenye utajiri wa shaba, ambapo kuna ukosefu mkubwa wa ajira.

Katika kampeni alikuwa pia akisema kwamba, Zambia inahitaji kiongozi anayeelewa biashara na anayeweza kugeuza uchumi ili kufungua faida za maendeleo katika afya, elimu na nyanja zinginezo.

Alitumia pia mizizi yake ya kilimo kuwavutia wakulima wa nchi hiyo, akisema anaweza kugeuza Zambia kuwa shamba linalotegemea na ukada huo, hususani kwa nchi tajiri zinazopakana na Zambia za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Namibia.

Rais huyu mpya wa Zambia alizaliwa katika familia ya kawaida na katika maisha yake ya utotoni alikuwa mchunga ng’ombe za familia.

Baada ya kwenda shule alijiunga na Chuo Kikuu cha Zambia kwa ufadhili wa serikali na kuhitimu masomo yake mwaka 1986 ya Shahada ya Sanaa (BA) katika Uchumi na Biashara.

Baadaye alipata shahada ya uzamili ya somo la Fedha na Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza. Tangu wakati huo, Hichilema, anayejulikana kwa upendo, amekuwa na rekodi ya kuvutia katika biashara, ndani na nje ya taifa hilo.

Hichilema, Anatajwa kuwa mmoja wa wauzaji wakubwa wa nyama katika soko la ndani la Zambia, na pia mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa zaidi nchini Zambia wanaouza nje ya nchi bidhaa zitokanazo na mifugo.

Pia ana uwekezaji mkubwa katika sekta ya utalii ya Zambia. Kufuatia elimu yake ya Chuo Kikuu, Hichilema kabla ya kugeukia biashara aliwahi kushika madaraka ya juu katika makampuni mbalimbali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz