Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndio Waziri anakwepa kupeana mkono na Wanawake

Hamza Abdi Barre Waziri Mkuu wa Somalia, Hamza Abdi Barre

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Somalia, Hamza Abdi Barre, amekuwa na tabia ambayo wengi wamekuwa wakijiuliza ni nini chanzo cha yeye kufanya hivyooo?

Tabia hii ambayo si ngeni kwa wanaoumjua ni ile ya kutowasamilia wanawake 'kwa mkono' popote pale anapokutana nao iwe kwenye dhifa za kitaifa au eneo lingine lolote.

Tukio ambalo limezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni, ni lile linalomuonyesha mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Catriona Laing, akiinua mkono wake kumsalimia Waziri Mkuu huyo lakini akaukwepa na kurudisha salamu kwa kuweka mkono kifuani.

Kupitia mitandao ya kijamii wengine wameonyesha kukosoa uamuzi wa Barre, huku wengine wakiunga mkono wakisema inatokana na sababu za kidini.

Baadhi ya waislamu hawapeani mikono na wanawake ambao si wake zao, wanaamini ni dhambi kuwagusa wanawake wasio wake zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live