Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu ya mkosoaji mkuu wa Rwanda kutoka leo

Kigaliiii Hukumu ya mkosoaji mkuu wa Rwanda kutoka leo

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: BBC Swahili

Mahakama mjini Kigali leo inatarajia kutoa hukumu yake dhidi ya Paul Rusesabagina, mkosoaji mkuu wa serikali ya Rwanda pamoja na wenzake 20 wanao tuhumiwa kwa makosa ya ugaidi . Tuhuma hizo zinahusishwa na mashambulio yaliyofanywa na kundi la waasi la MRCD-FLN dhidi ya Rwanda kati ya mwaka 2018 na 2019.

Waendesha mashtaka katika kesi hiyo waliomba mpinzani huyo kupewa hukumu ya kifungo cha maisha mara tu kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa kwa madai kuwa hawezi kupata haki katika mahakama za Rwanda kufuatia madai ya awali aliyoanza kuhusishwa.

Aidha , Juhudi za Bwana Paul Rusesabagina ambaye ni mwanahotelia wa zamani zilisaidia kuwaokoa zaidi ya watu 1200 wakati wa mauaji ya kimbari nchini humo ziliangaziwa katika filamu ya Marekani, Baadaye alikuwa mkosoaji wa serikali ya Rais Paul Kagame.

Chanzo: BBC Swahili