Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu ya kukufuru dhidi ya Mnigeria asiyeamini kuna Mungu yapunguzwa

Hukumu Ya Kukufuru Dhidi Ya Mnigeria Asiyeamini Kuna Mungu Yapunguzwa Hukumu ya kukufuru dhidi ya Mnigeria asiyeamini kuna Mungu yapunguzwa

Tue, 14 May 2024 Chanzo: Bbc

Mubarak Bala, Mnigeria asiyeamini kuwa kuna Mungu ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 24 jela kwa makosa yanayohusiana na kukufuru mwaka 2022, amepunguzwa kifungo hicho hadi miaka mitano baada ya kukata rufaa.

Kulingana na wakili wa Bala, James Ibori, jopo la majaji watatu katika jimbo la Kano liliamua kwamba hukumu ya awali ilikuwa "kali zaidi" na "kinyume na vifungu vya sheria".

Haijulikani ni lini Bala, ambaye amekuwa gerezani kwa miaka minne, huenda akaachiliwa.

Kesi yake ilizua hasira ya kimataifa alipokamatwa mwaka wa 2020.

Kundi la Waislamu lilikuwa limewasilisha ombi kwa mamlaka likimtuhumu Bala kwa kuchapisha ujumbe wa kukashifu Uislamu kwenye mitandao ya kijamii.

Baadaye alikiri mashtaka yote 18 na akahukumiwa kifungo cha miaka 24 jela na mahakama kuu katika jimbo la Kano kaskazi mwa Nigeria, lenye Waislamu wengi.

Kumekuwa na miito kadhaa ya kushinikiza kuachiwa kwa Bala na kuzuiliwa kwake kumezua hofu kuhusu uhuru wa kujieleza nchini Nigeria.

Chanzo: Bbc