Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma za treni zasitishwa kabla ya maandamano ya Kenya

Huduma Za Treni Zasitishwa Kabla Ya Maandamano Ya Kenya Huduma za treni zasitishwa kabla ya maandamano ya Kenya

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Shirika la Reli la Kenya limesitisha shughuli zake zote za treni ya abiria katika mji mkuu, Nairobi, kabla ya maandamano ya kupinga serikali Jumatatu yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Katika taarifa ya Jumapili, usimamizi wa Shirika la Reli la Kenya ulihusisha uamuzi huo na "hali zisizoweza kuepukika."

"Tunaomba radhi kwa wateja wetu wote kwa usumbufu wowote uliojitokeza," ilisema.

Hata hivyo, mwendesha treni alisema treni zake zote za abiria kati ya stesheni ya zamani ya reli katikati mwa jiji (Kituo Kikuu cha Nairobi) hadi kituo cha reli cha Nairobi-Mombasa (Nairobi Terminus) - zitaendesha jinsi ilivyoratibiwa.

Muungano wa upinzani unafanya maandamano jijini Nairobi na maeneo mengine ya nchi kushinikiza mageuzi ya uchaguzi na kupunguzwa kwa bei ya bidhaa za kimsingi.

Siku ya Jumapili, mkuu wa polisi alipiga marufuku maandamano hayo, lakini upinzani umeshikilia kuwa maandamano hayo yatafanyika kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: Bbc