Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huawei yaunga mkono malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa

B0fc55d31788d9f3699656e21e6f4d68 Huawei yaunga mkono malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPUNI ya mawasiliano ya Huawei imeunga mkono malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) katika kujenga ulimwengu wa kijani, ubunifu na umoja ikiwa kampuni hiyo pia inaamini teknolojia inaweza kufanya kazi kama injini ya maendeleo ya binadamu.

Akizungumza katika Mkutano wa masuala ya Ushirikiano, ukuaji na Ufanisi katika masuala ya teknolojia uliofanyika Shanghai, Makamu wa Rais mwandamizi wa Huawei na mjumbe wa bodi, Catherine Chen, alisema teknolojia inaweza kuwa injini ya maendeleo ya binadamu na akatoa wito kwa watu binafsi na wafanyabiashara kufikiria mambo kwa ukubwa zaidi na kutenda kidogo.

Chen alisema ni muhimu kwamba watu wawe karibu zaidi na teknolojia, ambayo kimsingi inaweza kuwa nguzo sahihi ya kufanikiwa kufikia malengo ya maendeleo.

"Mabadiliko makubwa ya kijamii huwa yanatokea kwa njia ya kuambukizana na mafanikio katika sayansi na teknolojia. Lakini leo, maendeleo ya kiteknolojia yanayoripotiwa ni ya kisiasa - kama wakati mwingine imekuwa hivyo kwa teknolojia 5G,"alisema.

Chen alisema teknolojia ya 5G ilikuwa teknolojia sanifu iliyofafanuliwa na upeo wake wa juu na muunganisho mpana, ambao unaweza kubadilisha tasnia za awali na kufaidisha wote.

"Kila siku, watumiaji wananufaika na ufanisi wa teknolojia ya 5G, wakati matumizi ya viwandani kwenye bandari, migodi na sekta ya uchukuzi inaongeza ufanisi wa utendaji,"alisema.

Chen alisema kila wakati kumekuwa na tishio kwamba teknolojia mpya inaweza kutumiwa vibaya, sheria zinaweza kuanzishwa kudhibiti hatari za kiteknolojia.

"Watu wengi tayari wana bidii kazini kuunda sheria za utawala kwa usalama wa mtandao, ulinzi wa faragha, yote ambayo yatatuweka salama. Kwa sisi wengine, ni wakati wa kujiamini na kufungua maendeleo ya teknolojia,"alisema.

Chen alielezea jinsi Huawei ilivyo tayari kupeleka suluhisho za kidijiti kuwawezesha watu na kufikia malengo ya maendeleo ya UN - hasa malengo ya uvumbuzi, usawa na elimu bora.

Nchini Afrika Kusini, kwa mfano, Huawei, shirika lisilo la faida la Click Foundation waliungana na kuunganisha zaidi ya shule 100 za msingi za mijini na vijijini kwenye huduma za intaneti. Lengo ni kuongeza ujuzi wa kusoma na kuziba pengo la dijiti kupitia teknolojia.

Nchini Kenya, Huawei ilishiriki katika kujenga Digitrucks, vyumba vya madarasa vinavyotumia umeme wa jua ambavyo huleta ustadi wa kidijiti kwa jamii za pembezoni , ambazo hazina huduma hiyo.

Chen pia alielezea namna Huawei Smart PV ivyotumiwa katika nchi zaidi ya 60 ikiwa tayari imesaidia kufikia SDGs, na imepunguza uzalishaji wa kaboni kwa tani milioni 148.

“Hii ni sawa na kupanda miti zaidi ya milioni 200. Nchini Ethiopia pekee, tumesaidia wateja wetu kupeleka zaidi ya vituo 400 vya umeme wa jua, kupunguza uzalishaji wa kaboni kwa tani 2,850. Nchini China, tumesaidia pia kujenga vituo vikubwa zaidi vya jua maalum kwa kilimo na uvuvi katika miji wa Ningxia na Shandong. "

Huawei na UNESCO pia wameshirikiana kuzindua mpango wa shule huria kwa kuwezesha shule za Misri, Ethiopia na Ghana kuboresha ujuzi wao wa kidijiti kupitia elimu ya mtandaoni.

"Katika mifano hii yote kila unganisho, kila gramu ya uzalishaji imepunguzwa, kila wati ya umeme iliyookolewa, haingeweza kupatikana bila maendeleo madogo katika teknolojia," alisema Chen.

Chanzo: habarileo.co.tz