Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hotuba ya Ramaphosa yadaiwa kuandikwa kwa ChatGPT

Ramaphosa  Dilemma Hotuba ya Ramaphosa yadaiwa kuandikwa kwa ChatGPT

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Rais nchini Afrika Kusini inachunguza kubaini kama ni kweli sehemu za hotuba ya Rais Cyril Ramaphosa aliyoitoa juma lililopita iliandikwa kwa kutumia programu ya akili mnemba (AI) ya ChatGPT.

Taarifa kwa vyombo vya habari nchini humo vimeeleza kuwa sehemu za hotuba hiyo iliyotolewa katika jukwaa la elimu hazikuandikwa na Rais au waandishi wa hotuba.

Msemaji wa Rais, Vincent Magwenya amekanusha madai hayo na kueleza kuwa hawatumii akili mnemba kuandika hotuba.

Amesema kuwa sehemu ya hotuba hiyo iliandikwa na idara ya elimu, na kuongeza kuwa wanafuatilia kujua chanzo cha hotuba hiyo, akisisitiza kuwa matumizi ya AI kuandaa hotuba au mifumo mingine ya kompyuta haikubaliki.

"Hatua zitachukuliwa endapo madai haya yatathibitika kuwa ni kweli". Magwenya ameeleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live