Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali zaanza kutoa matibabu Libya

Maiti Zazagaa Katika Mitaa Ya Derna, Huku Misaada Ikimiminika Libya Hospitali zaanza kutoa matibabu Libya

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa afya wa serikali yenye makao yake mashariki mwa Libya ametangaaza kuwa, huduma zimeanza kutolewa tena katika hospitali sita za mji wa Derna, ikiwa ni wiki moja baada ya kimbunga na mafuriko mabaya kuyapiga maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.

Waziri Othman Abdul Jalil amewaambia waandishi wa habari mjini humo kwamba, Kamati ya Matukio ya Dharura imefanikiwa kufungua hospitali sita katika mjini wa wa Derna kwa ajili ya upasuaji na kwa kuongezea ni kwamba hivi sasa hospitali hizo zinatumia vifaa vya kisasa katika huduma zao.

Afisa huyo ameongeza kuwa, wananchi wa kawaida, waokoaji na watu wa kujitolea mjini Derna wote wamepigwa chanjo za kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza. Hatua nyingine zilizochukuliwa ni kuundwa kamati ya kutoa msaada wa kisaikolojia kwa waathirika wa mafuriko katika mji huo ambao ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa vibaya na mafuriko. Mji wa Derna uko umbali wa kilomita 1,300 mashariki mwa mji mkuu Tripoli.

Tarehe 10 mwezi huu wa Septemba, kimbunga cha Daniel kilisababisha mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini Libya katika miongo kadhaa iliyopita. Hadi sasa zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine 10,000 hawajulikani walipo. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu rasmi za serikali ya Libya. Mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga cha Daniel yamesababisha maafa makubwa sana nchini Libya

Libya ina utajiri mkubwa wa mafuta lakini haina serikali kuu yenye nguvu na kwa miaka mingi sasa inatawaliwa na serikali mbili hasimu za mashariki na magharibi. Hali hiyo imekuja baada ya kuangushwa utawala wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Wakati huo huo mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amesisitizia umuhimu wa kuongezwa na kuharakishwa juhudi za pamoja za kuikwamua Libya kutokana na maafa ya mafuriko hayo makubwa yaliyoiyakumba maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo wiki iliyopita.

Abdoulaye Bathily alisesema hayo jana Jumapili wakati alipoonana na Mkuu wa Baraza la Uongozi la Libya, Mohamed Menfi katika mji mkuu Tripoli, ambapo alitoa rambirambi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kufuatia mafuriko yaliyosababisha maafa makubwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live