Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Kitaifa Kenya yafanya upandikizaji wa figo unaohusisha upasuaji kidogo sana

Hospitali Ya Kitaifa Kenya Yafanya Upandikizaji Wa Figo Unaohusisha Upasuaji Kidogo Sana Hospitali ya Kitaifa Kenya yafanya upandikizaji wa figo unaohusisha upasuaji kidogo sana

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Hospitali kubwa zaidi ya rufaa nchini Kenya, Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, imefanya upandikizaji wa figo kwa njia ya laparoscopic, na kuwa kituo cha kwanza cha umma nchini humo kufanya upasuaji wa upandikizaji wenye kuhusisha upasuaji mdogo sana tumboni.

Upandikizaji huo ulifanyiwa kwa Dickson Njoroge mwenye umri wa miaka 36, ​​ambaye alipokea figo kutoka kwa binamu yake.

Utaratibu huo hutumia chale ndogo kutoa na kupandikiza figo, kwa kusaidiwa na zana maalum kama vile kamera za ukuzaji zinazoongozwa na kompyuta.

Ni tofauti na upandikizaji wa kawaida wa figo wa wazi, ambao unahitaji chale kubwa kwa wapokeaji na wafadhili wa figo.

Hospitali hiyo inasema kuwa Wakenya hawahitaji tena kusafiri nje ya nchi kufanyiwa upasuaji huo.

Dk Charles Waihenya na Dkt Paul Njogu, madaktari bingwa wa upasuaji, walisema kuwa upandikizaji wa laparoscopic wa figo hutoa faida nyingi, ikiwa ni pamoja na maumivu kidogo, kupoteza damu kidogo, kupona haraka, gharama nafuu na matokeo bora.

Upandikizaji wa figo kwa njia ya Laparoscopic ni jambo la kawaida katika sehemu nyingi za dunia lakini bado haujakubaliwa sana katika nchi za Afrika kutokana na mapungufu katika miundombinu ya afya na utaalamu wa upasuaji.

Chanzo: Bbc