Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Homa ya nyani walipuka Congo DR

Nyani Msz Homa ya nyani walipuka Congo DR

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nyani (mpox), baada ya watu 19 kuthibitishwa katika miji mitano ikiwa ni pamoja na mji mkuu Kinshasa kuugua ugonjwa huo.

Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Gilbert Mokoki amesema hakuna vifo vilivyorekodiwa kufikia sasa, lakini ametoa wito kwa umma kuchukua tahadhari kwa kukaa mbali na watu wanaoshukiwa kuambukizwa homa hiyo, kuepuka kukaribiana na wanyama na kutoshika nyama za wanyamapori kwa mikono mitupu.

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), homa ya nyani iligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa binadamu katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1970. Dalili zake ni pamoja na homa kali,maumivu na vidonda kwenye ngozi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live