Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Homa ya Dengue yaua zaidi ya watu 350 Burkina Faso

Homa Ya Dengue Homa ya Dengue yaua zaidi ya watu 350 Burkina Faso

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ugonjwa wa homa ya Dengue, ugonjwa unaoenezwa na mbu, umeua watu 356 nchini Burkina Faso kati ya katikati ya mwezi wa Oktoba na katikati ya mwezi wa Novemba, na kufanya idadi ya vifo kufikia 570 tangu Januari 1, taasisi kutika Wizara ya Afya imetangaza siku ya Ijumaa.

Kuanzia Januari 1 hadi Novemba 19, "watu 123,804 wanaoshukiwa kuambukizwa homa ya Dengue) waliripotiwa, ikiwa ni pamoja na wagonjwa 56,637 pamoja na vifo 570, vilivyorekodiwa na Kituo cha Operesheni za Dharura za Afya (Corus), ametangaza mkurugenzi wake, Joseph Soubeiga, wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Kufikia Oktoba 15, chanzo hicho kiliripoti vifo 214 tangu kuanza kwa mwaka huu. Kati ya Oktoba 15 na Novemba 19, watu 356 walikufa kutokana na homa ya Dengue. Kuanzia Novemba 13 hadi 19 pekee "vifo 59 vilirekodiwa", ameongeza Bw. Soubeiga, ambaye amebainisha kuwa katika kipindi hicho, "watu 13,896 wanaoshukiwa kuambukizwa homa ya Dengue walijulishwa, ikiwa ni pamoja na wagonjwa 6,829" na "wagonjwa 1,101 waliokuwa katika hali maya waliolazwa hospitalini".

Ili kujaribu kuzuia kuendelea kwa janga hili, serikali imezindua kampeni ya kunyunyizia dawa za mbu katika miji miwili iliyoathiriwa zaidi: mji mkuu Ouagadougou (katikati) na Bobo-Dioulasso (magharibi). "Nyumba za wagonjwa 1,642 na nyumba za majirani" na "nafasi 696 za umma" zimeshughulikia, ameongeza.

Burkina Faso imekuwa na visa vya homa ya Dengue tangu miaka ya 1960, lakini janga lake la kwanza lilirekodiwa kuanzia mwaka 2017, na vifo 13. Huambukizwa kwa kuumwa na mbu aliyeambukizwa, kama vile malaria inayoonyesha dalili zinazofanana, Dengue ni kirusi kilichoenea katika nchi zenye joto jingi, ambacho hutokea hasa katika maeneo ya mijini na nusu mijini, na kusababisha vifo vya milioni 100 hadi 400. Maambukizi kila mwaka , kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Homa ya Dengue inaweza kusababisha homa kali, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kutapika, maumivu ya misuli na, katika hali mbaya zaidi, kutokwa na dam, hali ambayo inaweza kusababisha kifo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live