Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Homa ya Dengue yaua watu 750

Fv Dengue Homa ya Dengue yaua watu 750

Sun, 26 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya ya Burkina Faso, imesema ugonjwa wa homa ya Dengue au 'Kidingapopo' unaoenezwa na mbu, umeua watu mia tatu hamsini na sita nchini humo kati ya mwezi wa Oktoba na katikati ya mwezi wa Novemba mwaka huu na kufanya idadi ya vifo kufikia mia tano sabini tangu Januari Mosi.

Kituo cha Operesheni za Dharura za Afya kimesema kuanzia Januari Mosi hadi Novemba 19, watu laki moja, elfu ishirini na tatu, mia nane na wanne, walioshukiwa kuambukizwa homa hiyo waliripotiwa, wakiwemo wagonjwa elfu hamsini na sita, mia sita thelathini na saba na vifo mia tano sabini vilivyorekodiwa.

Ili kuzuia janga hilo, serikali imezindua kampeni ya kunyunyizia dawa za mbu katika miji miwili iliyoathiriwa zaidi ukiwemo mji mkuu Ouagadougou na Bobo-Dioulasso, Magharibi mwa nchi hiyo  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live