Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hofu yatanda mwanaume anayeomba kumuua Mkuu wa UN Sudan

Hofu Yatanda Mwanaume Anayeomba Kumuua Mkuu Wa UN Sudan Hofu yatanda mwanaume anayeomba kumuua Mkuu wa UN Sudan

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Umoja wa mataifa unasema una wasiwasi mkubwa kuhusu video ya mwanaume ambaye anaomba idhini ya kidini kumuua mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan.

Kwa hasira kubwa, mwanaume huyo anamshutumu muwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Volker Perthes kuingilia siasa za nchi.

Umoja wa Mataifa umezitaka mamlaka za Sudan kuchunguza tukio hilo.

Sudan imo katika mzozo wa kisaisa baada ya viongozi wake wiki hii kushindwa kuunda serikali inayoongozwa na raia katika muda uliopangwa.

Tofauti kati ya makundi ya kijeshi zimekuwa pingamizi kwa mazungumzo ya mageuzi yanayoendelea

Rekodi ya video hiyo ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha mwanaume mkongwe Msudan akimtusi afisa wa Umoja wa Mataifa na pia akiomba fatwa ya kuuliwa kwake.

Tukio hilo lilitokea wakati wa mkutano ulioitishwa na vyama vya Kiislamu vyenye uhusiano na kion rais wa zamani aliyepinduliwa, Omar Al Bashir.

Katika taarifa, waandalizi walisema kauli za mwanaume huyo haziwakilishi maoni yao.

Mwaka jana, maelfu ya waandamanaji wa Kiislamu walimtaka balozi wa Ujerumani kuondokanchini sudan, wakimshutumu yeye na Umoja wa Mataifa kwa kuingilia siasa za ndani ya nchi.

Sudan imekabiliwa na karibu maandamani ya kila wiki tangu utawala wa kijeshi unaoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan unyakue mamlaka kutoka kwa serikali ya kiraia mwezi Oktoba, 2021.

Mazungumzo kwa ajili ya jeshi kukabidhi mamlaka kwa serikali inayoongozwa na raia yamekwama kutokana na tofauti ndani ya makundi ya kijeshi.

Chanzo: Bbc