Raia wa Sudan Kusini waliokimbia vita kati ya mwaka 2013 na 2016 wamekatishwa tamaa kurudi nyumbani kwa sababu wanajeshi bado wanakaa katika nyumba zao, wachunguzi wa amani wamesema.
Luteni Jenerali Asrat Denero Amad, jenerali wa jeshi la Ethiopia ambaye anaongoza timu ya ufuatiliaji wa usitishaji mapigano, aliwaambia wanachama kwamba makumi ya nyumba za raia bado zinakaliwa na vikosi vya serikali. Ingawa hakuonesha maeneo ya majengo yaliyochukuliwa na wanajeshi.
Jenerali Asrat alisema uvamizi wa nyumba za askari wa serikali ulikuwa unazuia kuanza tena kwa maisha ya kawaida.
Makamanda wa vikosi vya ulinzi vya Sudan Kusini waliokuwepo wakati wa kongamano hilo ila hawakuzungumzia suala hilo.
Maelfu ya raia waliokimbia ghasia wakati wa vita bado wanaishi katika baadhi ya kambi zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa na wanasema hawawezi kurejea katika makazi yao.